Skip to main content

Posts

Showing posts from 2016

POLISI WAMTIA MBARONI ALOYEMCHOMA MKULIMA MKUKI MDOMONI

Wafugaji wa kijiji cha Changalawe kata ya Masanze wilaya Kilosa mkoani Morogoro walioyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kufuatia tukio la mkulima Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni hatimaye wamerejea makazini kwao huku wakilalamikia baadhi ya mifugo yao kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Wakizungumza baada ya kurejea kutoka porini walikojificha kwa siku tano wafugaji hao wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wamesema mtuhumiwa wa kosa la kumchoma mkuki mkulima wamemkabidhi kwenye mamlaka husika na hivyo wameliomba jeshi hilo kuwaacha huru wale wasiokuwa na hatia. Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema hawatasita kuwakamata wafugaji wote wanaoendelea kusababisha uvunjifu wa amani katika wilya ya Kilosa. Nao baadhi ya wakulima wamesema kijiji hicho kimekumbwa na hofu kubwa na kwamba familia ya ndugu Mtitu aliyechomwa mkuki nayo ilitoweka na kuomba hifadhi kwa wasa...

ALIKIBA AMESHINDA TUZO NCHIN FRANCE AKIWABWAGA DAVIDO,EDDY KENZO,SARKODIE,SERGE BEYNAUD,YEMIALADE

Fresh kutoka kushinda tuzo ya video bora ya mwaka (Aje) kwenye tuzo za Soundcity MVP za Nigeria, Alikiba ameongeza nyingine wikiendi hii. Mkali huyo ameshinda tuzo ya Chaguo la Watu (Prix du Public) kwenye tuzo za Ufaransa za Wana Music Awards zilizotolewa Ijumaa hii. “Hii ilikuwa ni tuzo pekee ambayo ilikuwa wazi kwa watu kupiga kura mwaka huu na msisimko uliozalishwa na tuzo hii umevuka matarajio yetu kwa kuwa na majadiliano zaidi ya 30,000 kwenye matangazo yetu kupitia mitandao ya kijamii,”  waandaji wa tuzo hizo Wana Corp wameandika kwenye tovuti yao. “Mshindi, Alikiba wa Tanzania aliweza kujikusanyia jamii kubwa ya mashabiki, ‘mashabiki damu wa Alikiba’ kuweza kuuchukua ushindi. Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa Alikiba akiwa na sahihi katika label kubwa ya Sony, kushinda tuzo ya kimataifa ya MTV Europe Music Awards kama ‘Best African Act’ na yote kwa yote kuwa na moja ya video bora za mwaka na Aje,” wameongeza. “The main information of this “Public Prize” is t...

MANENO YA RAPA NIKKIMBISHI KUHUSU HALI YA CHID BENZ

Leo December 30, 2016 rapa Nikki Mbishi amefunguka kuhusu watu wanaolalamika kuhusu hali ya rapa anayetawa kuwa mkali wa Freestyle Tanzania, Rashid Makwilo a.k.a Chid Beenz a.k.a Chuma a.k.a Chid wa Ilala na kusema kwamba watu wengi wanaolalamika hawajui ukweli kuhusu Chid. Nikki Mbish amesema tatizo la Chid Benz amekuwa hataki kusikia lolote kutoka kwa watu wanaohitaji kumsaidia, na kila akisaidiwa kupelekewa Rehab anatoroka, lakini pia watu wanaompiga picha wengi wao hawajui matatizo ya Chid na wanataka kuonekana tu walikuwa naye. Unaweza kusoma kila kitu alichokiandika hapa chini kupitia Instagram. “Siwezi kupost hata picha yake wala video maana ni   #FEDHEHA   tu ila ukweli ni kwamba nafsi ya   #CHID_BENZ   haiko tayari kusaidiwa kuacha   #NGADA .  Kwanza kila ukikutana naye anataka aongee yeye tu maneno yake ya   #LAWAMA   na kujiona anaonewa ili hali ana   #HAKI   sana bila kujali hali aliyonayo kwa sasa. Kuna waathirik...

SIKUJITANGAZA KUWA MIMI BADO NI BIKIRA ILA ILITOKEA TUU-CHEMICAL

Rapper Chemical amedai kauli yake ya kuwa yeye bado ni bikira (bado hajaupoteza usichana wake) umewafanya wanaume wengi kumtokea huku watu wengine wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume. Chemical amedai wakati anatoa kauli hiyo hakudhamiria kuweka wazi suala hilo lakini alilazimika kutoa jibu hilo baada ya kuulizwa swali. “Kiukweli toka nimefanya vile napata comment nyingi sana wengine wanasema sikuwa na busara kufanya vile,” Chemical alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Lakini nataka kuwaambia kwanza sikujitangaza ila ilitokea tu baada ya kuulizwa vitu ambavyo inawezekana siwezi kuvijibu,” Aliongeza, “Lakini napenda kuwaonyesha watu tusilazimishe kwa kuwa wewe umepitia kitu fulani wote tunatakiwa kuwa tumepitia jambo hilo, mimi najua background yangu niliyotokea siku zote na focus kwenye ‘Career’ yangu sitaki kitu chochote kiniharibie hasa sijui mwanaume ajae kuniharibia maisha yangu” alisema Chemical Mbali na hilo Chemical aliweka wazi juu ya watu ambao wamek...

RIPORT JOSE MOURINHO AMEBADILISHA MAWAZO JUU YA LINDELOF

Likija swala la kuripoti ishu za usajili BBC wamejipatia standard ya juu kwasababu mara nyingi huwa hawakosei juu ya ishu za usajili. Sasa hivi wameripoti kwamba Mourinho amebadirisha mawazo yake juu ya kumsajili mchezaji Victor Lindelof kutoka Benfica. Imeripotiwa sana kuhusu mchezaji huyu kuelekea kujiunga na club ya Manchester united ambapo ali saini hadi jezi ya Manchester ambayo alikuwa nayo shabiki mmoja. BBC wameandika kwamba Jose ameshawishiwa kwa uzuri wa Rojo na Jones kwenye ulinzi sehemu ya kati kati kiasi cha kubadirisha maamuzi ya kutaka kumnunua mchezaji huyo. Jose pia ana imani kubwa na Eric Bailly, Chris Smalling na Daley Blind. Lindelof ilitoka taarifa kwamba zingetuma Euro millioni 45 ili awezeze kuhamia Manchester United kutoka Benfica, Kiasi hiki kingekua kikubwa zaidi kwa Benfica tangu waanze kuuza wachezaji.

NAVY KENZO KUIZINDUA ALBAMU YAO IITWAYO ABOVE IN A MINUTE JUMAMOSI

Navy Kenzo wataizindua rasmi album yao mpya, ‘Above In A Minute’ Jumamosi hii, December 31 . Uzinduzi huo utafanyika kwenye ukumbi wa Hyatt Regency Level 8 jijini Dar es Salaam. Nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Lini waliyomshirikisha Alikiba, Bajaj waliyomshirikisha msanii wa Nigeria, Patoranking, Done wakiwa na Mr Eazi, Morning, Bless Up wakiwa na msanii wao, Rosa Lee, Nipendelee wakiwa na kundi la Ghana, R2Bees na zingine. Wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo ni Feel Good waliyomshirikisha Wildad ambao ulitoka na video zake.  Kwa kiasi kikubwa album hiyo imetayarishwa na Nahreel huku Chizan Brain akifanya mixing na mastering. Watayarishaji wengine waliohusika kuisuka AIM ni pamoja na Chostix aliyetayarisha wimbo ‘Done’ pamoja na DJ Moshe Buskila aliyetayarisha nyimbo mbili.

LIST YA WASHINDI WA WATSUPTV AFRICA AWARDS 2016 GHANA WATANZANIA WAKO WANNE

Usiku wa December 28 2016 tuzo za  WatsUp TV Africa Music Video Awards 2016  ndio zilitangazwa  Accra Ghana , washindi 22 walitangazwa kupitia  Press Conference  wakiwemo wasanii wa  Tanzania  waliyofanikiwa kushinda tuzo hizo kwa mwaka 2016. Kama hufahamu  WatsUp TV Africa Music Video Awards  (WAMVA) ni tuzo ambazo zinaandaliwa na  WatsUP TV , zikiwa na lengo la kushawishi au kuhamasisha wasanii kufanya video za viwango vya juu pamoja na ubora. Wametangazwa washindi 22 wasanii na waongozaji wa video 170 waliyokuwa wametajwa kuwania tuzo hizo wakati zinazinduliwa mwezi September 2016,  kwa mujibu wa mtandao wa  Zionfelix.net  ni kuwa washindi watafanya show katika tamasha la  Made in Africa  litakalofanyika 2017  Accra Ghana . List ya washindi wote 22 waliyotangazwa Best Newcomer Video of the Year Harmonize   ft  Diamond Platinium   ( Badoo) Best African Reggae Da...

WASANII AMBAO WANATAKIWA KUANGALIA SANA 2017

Billboard  ni moja kati ya partners wakubwa sana kwenye muziki duniani, pia wanahusika na upangaji wa chart kubwa zaidi duniani za muziki kupitia mtandao wao, leo ninayo hii kutoka kwao ambapo wameitoa list ya wasanii 10 wanaoanza kufanya vizuri kwenye muziki, jina la star muimbaji  Tekno  limewekwa kwenye list hiyo. Wasanii hao ni kutoka sehemu zote duniani na kupitia list hiyo, Tekno ndiye msanii pekee kutoka  Afrika  aliyetajwa kuwemo kati ya wasanii 10 wa kuwaangalia zaidi mwaka 2017 na wote wanafanya muziki wa  Hip-Hop   na  R&B. jarida la  Billboard  pia limethibitisha deal iliyosainiwa kati ya Tekno na kampuni kubwa ya kusambaza muziki duniani  “Sony Music”  ambapo yeye atakuwa chini studio za  Columbia Records. Billboard  wameandika: “Tekno tayari ana hits kali nchini kwake Nigeria, na Columbia Records wanafahamu hilo, huyu ni msanii mzuri, na ana sauti yenye kuvutia kila...

MUDA WA DIRISHA DOGO MOURIHNO ATAWAFUNGULIA MILANGO WACHEZAJI HAWA HAPA

Tukikaribia muda wa dirisha dogo tunategemea kuona movement ya wachezaji wengi kwenda kwenye timu mbali mbali wakiziacha timu zao za sasa hivi. Tangu afike Manchester united Mourihno amekua akisajili wachezaji ana kujaza nafasi za wachezaji wengi kwenye namba kadhaa kufanya wachezaji hao wote wakubwa wakigombania namba moja. Pia hadi sasa bado kuna tetesi za kuleta wachezaji wapya ambao wanakuja kuongeza swala la kugombani namba. Hivi sasa Manchester united inategemewa kumkalibisha mchezaji Victor Lindelog kutkka Benfica. Hawa ni wachezaji watano ambao huenda wasivae tena jezi ya Manchester united baada ya muda dirisha dogo kufika. Memphis Depay. Bila shaka huyu jamaa mwenye miaka 22 amepitia wakati mgumu kuonyesha uwezo wake ndani ya Old trafford tangu ahamie kutoka PSV. Depay amecheza dakika 22 tu tangu msimu huu wa uanze kwenye ligi. Hivi sasa anategemewa kujiunga na club ya Everton kwa mkopo ili akapate muda zaidi wa kucheza. Marouane Fellaini Fe...

LIST YA WACHEZAJI 48 BORA DUNIANI WA MUDA WOTE AFRIKA WAMETAJWA SABA

Ripoti mpya za  Shirikisho la Kimataifa la Historia ya Soka na Takwimu  (IFFHS)  zimeonesha list yenye majina ya mastaa 48 bora wa soka duniani wa muda wote ambao ni wakongwe na bara la Afrika limeingiza majina ya wachezaji 7 waliofanya vizuri kwenye mchezo huo. Wachezaji kutoka Afrika waliotajwa kwenye list hiyo ni pamoja na Nwanko Kanu (Nigeria), George Weah (Liberia), Lucas Radebe (Afrika Kusini), Mahmoud El-Khatib (Misri), Mohamed Aboutrika (Misri), Mustapha Rabah (Algeria) na Roger Milla (Cameroon).

AZAM YAACHANA NA MAKOCHA WAO WA HISPAINIA

Klabu ya  Azam FC  leo December 28 2016 imetangaza maamuzi ambayo hayakutarajiwa na wengi ya kuamua kuwafuta kazi makocha wake kutokea  Hispania ,  Azam FC  imewafuta wahispania waliyokuwa wanaounda benchi la ufundi la  Azam FC  wakiongozwa na kocha mkuu  Zeben Hernandes . Uamuzi wa  Azam FC  kuwafuta kazi makocha hao umefikiwa na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo, ambapo kwa siku za hivi karibuni wamekuwa hawapati matokeo ya kuridhisha. Kocha  Zeben Hernandes   anaondoka  Azam FC  akiwa kaiongoza timu hiyo katika michezo 17, akiwa kapata ushindi michezo saba pekee, sare michezo 6 na kupoteza michezo minne, akiwa kaiacha timu hiyo nafasi ya nne katika Ligi Kuu  Tanzania  bara ikiwa na point 27.

DARASSA AKIFANYA YAKE MBELE YA WAFANYABIASHA WA ILALA

Hit maker wa wimbo Muziki, Shariff Thabeet aka Darassa Jumatano hii alikutana na wafanyabiashara wa soko la Ilala Boma na kuonyesha baadhi ya vitu ambavyo ataenda kuvifanya Jumamosi hii kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam. Darassa akifanya yake mbele ya wafanyabiashara wa Ilala. Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane. Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo. Akiongea na mashabiki wake, Darassa alisema amejipanga vizuri kuonyesha mambo mapya katika jukwaa hilo la burudani. “Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila nin...

YANGA YA IFUNGA NDANDA FC GORI NNE BILA

Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 28 kwa Dar es Salaam Young Africans kuendelea na harakati zake za kutetea taji la Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa kuikaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam . Yanga ambao wamekuwa na rekodi sawa na Ndanda FC kwa mechi 5 zilizopita Yanga alikuwa kamfunga Ndanda mara moja na kufungwa mara moja huku wakiwa wametoka sare michezo mitatu, ila leo Yanga amefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0, magoli yakifungwa na Donald Ngoma dakika ya 4 na 21, Amissi Tambwe dakika ya 25 na Vincent Bossou. Mara ya mwisho Yanga kucheza na Ndanda FC ilikuwa ni September 7 2016 katika uwanja wa Nangwanda Sijaona Mtwara na mchezo ulimalizika kwa suluhu ya 0-0, kwa maana hiyo Yanga na Ndanda FC wamekutana mara 6, Yanga kapata ushindi mara mbili, kafungwa mara moja na sare tatu.

MSAANI WA MUZIKI WA HIPHOP BLACK RYNO AMEDAIWAKATI UMEFIKA WA MZIKI WA HIPHOP

Msanii wa muziki wa hip hop Black Rhyno amedai wakati umefika wa wasanii wa muziki wa hip hop kufanya vitu ambavyo vinapendwa. Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kama Movie’ akiwa amemshirikisha Jux, amedai tayari ameshafanya muziki wa kiharakati kwa muda mrefu na muda huu ni kwa ajili ya kufanya biashara. “Unajua muziki umekuwa ni biashara kikubwa ni kuubrand, tushafanya hizi za ‘dan Da daadah’ ila kuna wakati inabidi ufanye vitu watu wengi wanapenda,” Black Rhyno alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM. “Ndio maana tunafanya na hizi ngoma ambazo mambo yanazungumzwa zaidi kama mahusiano.” Black Rhyno ni miongoni kati ya marapa wakongwe ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa hip hop kwa muda mrefu bila kutetereka.

mke wa T.I aomba taraka

Headlines nyingine kutoka Marekani zimechukuliwa na mke wa rapper  T.I  kufungua rasmi kesi ya madai ya talaka kwa kile kinachosemekana kuwa amechoshwa na drama za  T.I  ambazo haziishi. Hii inakuja miezi michache tangu T.I kusema anaweza kumuacha mkewe kwa sababu alipiga picha na kucheza muziki na  Floyd Mayweather  ambaye ni hasimu wake. T.I na Tiny wamekuwa katika ndoa tangu mwaka 2010 na kufanikiwa kupata watoto watatu katika ndoa na wengine wanne nje ya ndoa hivyo wana jumla ya watoto saba.

SAMSON MAGOLI NI MFANYA BIASHALA YA MBWA JIJINI MWANZA

Inaweza kuwa nadra kusikia mtu akikwambia anataka kuanza biashara ya kuuza Mbwa ila ni biashara ambayo inafanywa na watu wachache na hawakosi senti zao.  i Samson Magoli  ambaye ni mkazi wa Mwanza, huingiza sio chini ya shilingi milioni mbili kwa mwezi na alianza kwanza kwa kuwapenda Mbwa na ni zaidi ya miaka mitatu toka aianze hii biashara. Mbwa wake wa kwanza kumuuza pesa nyingi alimuuza kwa shilingi milioni moja na laki nne, wengine kwa mwaka huu amekua akiwauza kwa shilingi laki moja na nusu mpaka laki mbili,

MTU ALIYEHUSIKA KWENYE SHAMBULIO LA LORI KATIKA SOKO LA CHRISTMAS

Mtu aliyehusika kwenye shambulio la lori katika soko la Christmas, Berlin na kuuawa watu 12 siku chache zilizopita ameuawa nchini Italia. Kijana huyo mwenye miaka 24 aliyetambulika kwa jina la Anis Amri raia wa Tunisia amedaiwa kuuawa na polisi wa mjini Milan baada ya kuwafyatulia risasi polisi waliotaka awaonyeshe vitambulisho vyake. Imedaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa hii kwenye eneo la Sesto San Giovani hata hivyo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kumuua polisi mmoja kabla na yeye kuuawa kwa kupigwa risasi.

NDEGE YA KIJESHI YA URUSI IMEPOTEA KWENYE RADAR DAKIKA CHACHE TUU'

Ndege ya kijeshi ya Urusi imepotea kwenye radar dakika chache tu baada ya kupaa angani kutoka kwenye mji wa Sochi. Add caption Wizara ya ulinzi imedai kuwa ndege hiyo, Tu-154 ilikuwa na watu 91 wakiwemo wanajeshi, bendi ya jeshi na waandishi wa habari. Ndege hiyo ilitoweka kwenye radar dakika 20 baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adler. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zimedai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaenda kwenye jimbo la Syria, Latakia. Msemaji wa wizara ya ulinzi, Igor Konashenkov amedai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaenda kushiriki kwenye mkesha wa mwaka mpya na wanajeshi wa Urusi walioko Syria. Majeshi ya Urusi, nchi yenye ukaribu na rais wa Syria, Bashar al-Assad yamekuwa yakifanya mashambulio dhidi ya makundi ya kigaidi.

SIMU ZENTE GHARAMA KUBWA DUNIANI MWAKA 2016

1 SHARE SHARE TWEET SHARE SHARE COMMENTS Simu za Smartphones zimekuwa ni kati ya vitu vinakimbizana na teknolijia kila kukicha, na ni moja kati ya vifaa ambavyo vimekuwa seheme ya maisha ya karibu asilimia 70 ya watu duniani lote, kuna wakati simu tunazomiliki zimekuwa zinatoa majibu ya wewe ni mtu wa aina gani. Simu zimekuwa zikitengenezwa kuleta ushindani wa teknolojia lakini kupima uwezo wa kifedha wa watumiaji na mapenzi. Kwa mujibu wa The Merkle wamezitaja aina 5 za simu ambazo mpaka kufikia mwezi December 2016 zimekuwa ni simu zilizovunja rekodi ya kuuzwa kwa bei ya juu kuliko simu nyingine zozote duniani. Japokuwa hizi simu ni za kawaida ila tu zimekuwa zikiongezewa urembo wa madini ya thamani kubwa ili kuzipa muonekano wa kipekee . 5.- GOLDVISH LE MILLION ($1.3 MILLION) (Zaidi ya Tsh. Bilioni 2.8) Sifa ya hii simu ukiishika kama sio mmliki wake inapiga kelele zenye sauti ya kuonesha imeibiwa. Cover la nje lote limeunda kwa Almasi y...