Skip to main content

Posts

Showing posts from April 13, 2017

Rais Magufuli amempigia simu Mwana FA

Jioni ya April 12 2017 staa wa muziki wa hip hop bongo   Hamisi Mwinjuma   ambaye wengi tunamfahamu kwa jina la   Mwana FA , alitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa twitter kuoneshwa kufurahisha na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania   John Pombe Magufuli   kumpigia simu. Mwana FA   ambaye kwa sasa anafanya vizuri katika radio na tv stations mbambali kwa hit single yake ya   Dume Suruali   amethibitisha kupigiwa simu na Rais kumwambi anakubali kazi zake. Kupitia ukurasa rasmi wa   twitter   wa staa huyo uliyokuwa verified aliandika   “nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais   @MagufuliJP   kunisalimia na kuniambia yeye ni mpenzi wa kazi zangu,haswa   #DumeSuruali ..”

LORD EYEZ AIKANA LEBO YA BANA YA BARAKAH THE PRINCE

Lord Eyez ameonekana kukataa kiaina kusainiwa na lebo ya BANA ambayo inamilikiwa na Barakah The Prince. Rapper huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya ‘Hela Yangu’ aliomshirikisha Jux, amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumsaini yeye kwakuwa ni mkubwa zaidi. “Kuna makubaliano yangu na Barakah chini ya BANA huo wino ni mimi na yeye, huo wino hamhusu mtu mwingine yeyote. Nafikiri kwa sababu hakuna mtu yeyote anaweza kuniown Lord Eyez. Hakuna mtu anaweza kumsaini Lord Eyez coz am too bigger for that,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV. “Nafikiri maswali yanakuwa mengi kwasababu labda watu hawakuniona Lord Eyez, hawakunipata nikizungumza. Unajua mimi sio mtu wa pele pele, mimi sio mtu wa kiki, mimi sio mtu wa media, mimi napenda muziki wangu uwe mkubwa kuliko mimi,” ameongeza.