Young Killer aeleza alivyojisikia baada ya Diamond kunukuu mistari minne kwenye nyimbo zake 3 tofauti
Diamond Platnumz ni shabiki mkubwa wa Young Killer. Na hitmaker huyo wa ‘Marry You’ si mtu anayesikiliza nyimbo za Msodoki juu juu tu, bali kwa undani kiasi cha kushika mistari kadhaa. Mwishoni mwa wiki, Diamond alionesha wazi kuzimia mistari konde ya rapper huyo wa Mwanza kwa kuandika minne kwenye post zake nne tofauti za Instagram na Twitter. Mistari ya Young Killer ambayo Diamond ameiandika kwenye post zake za Instagram ni pamoja na: 1. Asa Unataka kuwa mimi na mimi ntakuwa nani….? (Sinaga Swagga (Part1) 2. Naskia Usingizi ni Mbolea ndiomaana tukilala tunaota…? (Sinaga Swaga Remix) 3. Ukiona Nina changamoto changa Unga tusonge Ugali… Mwisho wa siku wote tunashiba, na Mambo yanakuwa shwari (Sinaga Swagga 1) 4. Shida ingekuwa sumu basi tungekufa wengine (Kumekucha f/ Mr Blue) “Binafsi nafarijika sababu ni [Diamond] mtu ambaye ana fan base kubwa kwahiyo anapokuwa ameshow love kwa kitu kama hicho kupost mistari yangu hata mashabiki wake pia wanakuwa wanan...