Tukikaribia muda wa dirisha dogo tunategemea kuona movement ya wachezaji wengi kwenda kwenye timu mbali mbali wakiziacha timu zao za sasa hivi. Tangu afike Manchester united Mourihno amekua akisajili wachezaji ana kujaza nafasi za wachezaji wengi kwenye namba kadhaa kufanya wachezaji hao wote wakubwa wakigombania namba moja. Pia hadi sasa bado kuna tetesi za kuleta wachezaji wapya ambao wanakuja kuongeza swala la kugombani namba. Hivi sasa Manchester united inategemewa kumkalibisha mchezaji Victor Lindelog kutkka Benfica. Hawa ni wachezaji watano ambao huenda wasivae tena jezi ya Manchester united baada ya muda dirisha dogo kufika. Memphis Depay. Bila shaka huyu jamaa mwenye miaka 22 amepitia wakati mgumu kuonyesha uwezo wake ndani ya Old trafford tangu ahamie kutoka PSV. Depay amecheza dakika 22 tu tangu msimu huu wa uanze kwenye ligi. Hivi sasa anategemewa kujiunga na club ya Everton kwa mkopo ili akapate muda zaidi wa kucheza. Marouane Fellaini Fe...