Skip to main content

Posts

Showing posts from January 23, 2017

DIVA AANGUKIA KATIKA PENZI LA MWANAMZIKI WA RNB HERIMZIKI

Diva The Bosslady ametufungulia hadi ndani ya ulimwengu wake mpya wa mapenzi . Amezama, ameoza katika penzi la msanii wa ‘Nakukumbukaga’, Heri Muziki. Jumapili hii ametumia Instagram kuonesha namna alivyokufa na kuzimia kwa muimbaji huyo. Mtangazaji huyo wa Clouds FM amepost video kadhaa akipeana mabusu ya kina Heri. Na hajaaacha kuandika maneno mazito kuonesha anavyompenda muimbaji huyo. “@herimuziki is The Key to My Happiness .. i chose to be Happy   My beib is so damn CUTE Mashaallah   #Lovebirds,” ameandika kwenye video moja. Kwenye nyingine ameandika, “@herimuziki is My Mr. perfect, The Most Handsome, My cute Pie , dope, sexy, Good Kisser , UGH YOUR My Perfect COMBO  YOUR MY WORLD, MY EVERYTHING  you make me so happy,I love you babe so much and I wanna Have your Cute Babies (twins) My Love     #LoveBirds Kwanza @soudybrown keshakupitisha .. hamna namna , shemeji yenu Guys stak maneno zaidi.” Kama kawaida, si wote w...

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.

SUMSUNG YATOA RIPORT YA KUHUSU SABABU ZA KULIPUKA KWA SIMU GALAXY NOTE 7

Kampuni ya Samsung imetoa taarifa yake baada ya kufanya uchunguzi juu ya sababu ya kulipuka kwa simu zake za Galaxy Note 7. Taarifa hiyo imebaini kuwa betri za simu hizo ndio zilizokuwa chanzo cha kulipuka kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye utengenezaji wa betri hizo ambazo zilitengenezwa na mbili ambapo ilitokana mwanzo katika uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa wake. Ripoti hiyo imeongeza kuwa matatizo mengine yalitokana na betri hizo kuwa kubwa na hivyo kutokaa vizuri katika sehemu yake ya ndani ya simu. Simu hizo zilisitishwa kuuzwa mwezi Oktoba mwaka jana huku ikikadiriwa kuwa simu hizo tayari zilikuwa zimeuza kiasi cha dola bilioni 5.3 duniani kote.

MCHEZAJI WA NICE YA UFARANSA AMESEMA ALIKUA MWATHIRIKA WA UBAGUZI WA RANGI

Mchezajiwa wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia. Balotelli ambaye mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26 aliandika katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua? ”Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa”. Balotelli ambaye alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya mechi waliyo toka sare ya 1-1 huko Corsica. Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo. Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote. Balotelli amesha funga mabao 10 katika mechi 15 tangu alivyo jiunga na ...