Skip to main content

Posts

Showing posts from February 13, 2017

VITA DHIDI YA MADAWA YA KULEVYA WATOTO HAWA WASIKITISHA WENGI VIDEO

Moja kati ya jambo lililowasikitisha wengi Jumatatu hii katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni pale walipotajwa watoto wawili wa kike ambapo mmoja ana umri wa miaka 14 na mwingine 16 kuwa walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa takriban miaka mitano. Wakati huo huo mtoto mmoja mwenye miaka 16 aliongeza kuwa mbali na kutumia madawa hayo lakini pia yamempelekea kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kuwa wakati mwingine ilimlazimu kujiuza ili apate fedha za kununulia dawa hizo. Wakati huo huo Kamishna mpya wa kupambana na Madawa ya kulevya, Rogers Sianga ameahidi kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia huduma bora za afya ambazo zitawasaidia wasirudi tena kwenye janga hilo. Orodha hiyo ya tatu iliyotolewa leo na Mh. Makonda ina idadi ya majina 97 ambapo kati yao amedai kuna majina ambayo yatawasha moto zaidi huku akiahidi kuwa kuna awamu nyingine nne zimebakia za kutoa majina hayo.

WAZIRI MKUU AAGIZA MAENEO YA MAGEREZA YAPIMWE

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa asimamie zoezi la upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na Magereza kote nchini na kuhakikisha yanawekewa mipaka. Ametoa agizo hilo leo mchana katika kikao baina ya Kamishna huyo mpya na Maafisa Magereza wa Mikoa yote na maafisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma. “Magereza yetu mengi yako kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na maeneo ya Magereza. Lazima tupime maeneo yote na kuyawekea alama mipakani ili kubainisha maeneo yetu,” amesisitiza. Mbali ya maeneo ya Magereza, Waziri Mkuu amesema, jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo amesema imechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi hilo. “Natambua kuwa jeshi hili lina mashamba makubwa lakini nayo pia hayajapimwa. Kila RPO ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapi...