MANJI AMWAGA MAMILION KWENYE GOOGLE ADS KUJISAFISHA SIKU MOJABAADA YA KUTAJWA KWENYE ORODHA MPYA YA MAKONDA
Siku moja baada ya mfanyabiashara maarufu na mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji kutajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye orodha ya pili ya watu wanaoshukiwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, amemwaga mamilioni ya fedha kulipia matangazo ya mtandaoni, google ads kujisafisha. Matangazo hayo yanaonekana kwenye tovuti nyingi, hata za nje unazozifungua kuanzia Alhamis hii. Hatua hiyo pia imekuja saa chache baada ya Manji kuitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia kutajwa kwake ambako alisema amedhalilishwa na kwamba ataenda polisi Alhamis hii badala ya Ijumaa kama ambavyo Makonda aliwataka. Matangazo hayo yanaonesha bango lenye picha yake na maelezo yasemayo ‘Yes I ‘am addicted to Yanga.’ Ukiclick, inakupeleka kwenye maelezo marefu yanayomwelezea mfanyabiashara huyo pamoja na mambo aliyoyafanya. Maelezo hayo ni kama yafuatayo: Manji Mwenyekiti wa kihistoria Yanga MWENYEKITI wa klabu ya soka ya Yanga ya Dar es Salaam, Yus...