Diamond ameingia choo cha kike kwa askofu Joseph Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Marry You’ amejikuta matatani baada ya kuachia wimbo mpya ‘Acha Nikae Kimya’ ambao umepokelewa vibaya na mashabiki wengi wa muziki. Katika wimbo huyo ametajwa askofu Gwajima kitu ambacho kimemchukiza mchungaji huyo maarufu katika mitandao ya kijamii. “Kesho Ibada itakuwa LIVE on YOUTUBE kuanzia saa nne na nusu, kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Kibo Dar es Salaam. Link itakuwepo kwenye Bio yangu. Usikose.,” aliandika Gwajima Instagram akiambatanisha na picha (hapo juu Baada ya ujumbe huo wa Gwajima, Diamond amerudi upya kuomba radhi kuhusu kumhusisha mchungaji huyo kwenye wimbo wake. “Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba ….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasi...