Skip to main content

‘Acha Nikae Kimya’ yamponza Diamond kwa Gwajima ‘Yala! yala! mwenzenu nimeyatimba’

Diamond ameingia choo cha kike kwa askofu Joseph Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima. Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Marry You’ amejikuta matatani baada ya kuachia wimbo mpya ‘Acha Nikae Kimya’ ambao umepokelewa vibaya na mashabiki wengi wa muziki.
Katika wimbo huyo ametajwa askofu Gwajima kitu ambacho kimemchukiza mchungaji huyo maarufu katika mitandao ya kijamii.
“Kesho Ibada itakuwa LIVE on YOUTUBE kuanzia saa nne na nusu, kutoka Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo Kibo Dar es Salaam. Link itakuwepo kwenye Bio yangu. Usikose.,” aliandika Gwajima Instagram akiambatanisha na picha (hapo juu
Baada ya ujumbe huo wa Gwajima, Diamond amerudi upya kuomba radhi kuhusu kumhusisha mchungaji huyo kwenye wimbo wake.
“Yala! Yala! Jamani Mwenzenu nimeyatimba😟….. lakini mi nafkiri watu wanatakiwa waiskilize hii nyimbo kwa umakini sana tena sana na wataelewa nini ilikuwa maana yangu haswa… Hususani kama kipengele nilichomtaja mzee wangu @Bishopgwajima nilisema: “mara nasikia vya aibu Konda na Gwajima eti ugomvi umekolea….ila kuchunguza kwa karibu ni kuna binti mmoja tu ndio kwa mitandao anachochea…”
Point yangu ni kwamba licha ya kweli kuna yaliyojiri nyuma, lakini kwa busara zao ninazoamini wamejaaliwa na Mwenyez Mungu muda si mref wangekaa chini na kumaliza…nawote kufurahi kwa pamoja, lakini kwakuwa kuna dada mwingine alikua anachochea hawa ndugu zetu wazidi kufarakana…ikapelekea hadi kufikia hapa…asa hapo kosa langu mie liko wapi?😭
Chonde chonde mzee wangu @Bishopgwajima usinigeuze maji kesho 👐, mana nakujua ukimuamulia mtu…. naweza jumapili ya kesho nikaiona chungu Mwaka mzima😁😆😅,” aliandika Diamond Instagram.

Comments

Popular posts from this blog

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.

MCHEZAJI WA NICE YA UFARANSA AMESEMA ALIKUA MWATHIRIKA WA UBAGUZI WA RANGI

Mchezajiwa wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia. Balotelli ambaye mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26 aliandika katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua? ”Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa”. Balotelli ambaye alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya mechi waliyo toka sare ya 1-1 huko Corsica. Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo. Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote. Balotelli amesha funga mabao 10 katika mechi 15 tangu alivyo jiunga na ...

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.