Skip to main content

Posts

Showing posts from December 25, 2016

SAMSON MAGOLI NI MFANYA BIASHALA YA MBWA JIJINI MWANZA

Inaweza kuwa nadra kusikia mtu akikwambia anataka kuanza biashara ya kuuza Mbwa ila ni biashara ambayo inafanywa na watu wachache na hawakosi senti zao.  i Samson Magoli  ambaye ni mkazi wa Mwanza, huingiza sio chini ya shilingi milioni mbili kwa mwezi na alianza kwanza kwa kuwapenda Mbwa na ni zaidi ya miaka mitatu toka aianze hii biashara. Mbwa wake wa kwanza kumuuza pesa nyingi alimuuza kwa shilingi milioni moja na laki nne, wengine kwa mwaka huu amekua akiwauza kwa shilingi laki moja na nusu mpaka laki mbili,

MTU ALIYEHUSIKA KWENYE SHAMBULIO LA LORI KATIKA SOKO LA CHRISTMAS

Mtu aliyehusika kwenye shambulio la lori katika soko la Christmas, Berlin na kuuawa watu 12 siku chache zilizopita ameuawa nchini Italia. Kijana huyo mwenye miaka 24 aliyetambulika kwa jina la Anis Amri raia wa Tunisia amedaiwa kuuawa na polisi wa mjini Milan baada ya kuwafyatulia risasi polisi waliotaka awaonyeshe vitambulisho vyake. Imedaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa hii kwenye eneo la Sesto San Giovani hata hivyo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kumuua polisi mmoja kabla na yeye kuuawa kwa kupigwa risasi.

NDEGE YA KIJESHI YA URUSI IMEPOTEA KWENYE RADAR DAKIKA CHACHE TUU'

Ndege ya kijeshi ya Urusi imepotea kwenye radar dakika chache tu baada ya kupaa angani kutoka kwenye mji wa Sochi. Add caption Wizara ya ulinzi imedai kuwa ndege hiyo, Tu-154 ilikuwa na watu 91 wakiwemo wanajeshi, bendi ya jeshi na waandishi wa habari. Ndege hiyo ilitoweka kwenye radar dakika 20 baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adler. Taarifa ambazo hazijathibitishwa, zimedai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaenda kwenye jimbo la Syria, Latakia. Msemaji wa wizara ya ulinzi, Igor Konashenkov amedai kuwa ndege hiyo ilikuwa inaenda kushiriki kwenye mkesha wa mwaka mpya na wanajeshi wa Urusi walioko Syria. Majeshi ya Urusi, nchi yenye ukaribu na rais wa Syria, Bashar al-Assad yamekuwa yakifanya mashambulio dhidi ya makundi ya kigaidi.