Leo December 30, 2016 rapa Nikki Mbishi amefunguka kuhusu watu wanaolalamika kuhusu hali ya rapa anayetawa kuwa mkali wa Freestyle Tanzania, Rashid Makwilo a.k.a Chid Beenz a.k.a Chuma a.k.a Chid wa Ilala na kusema kwamba watu wengi wanaolalamika hawajui ukweli kuhusu Chid. Nikki Mbish amesema tatizo la Chid Benz amekuwa hataki kusikia lolote kutoka kwa watu wanaohitaji kumsaidia, na kila akisaidiwa kupelekewa Rehab anatoroka, lakini pia watu wanaompiga picha wengi wao hawajui matatizo ya Chid na wanataka kuonekana tu walikuwa naye. Unaweza kusoma kila kitu alichokiandika hapa chini kupitia Instagram. “Siwezi kupost hata picha yake wala video maana ni #FEDHEHA tu ila ukweli ni kwamba nafsi ya #CHID_BENZ haiko tayari kusaidiwa kuacha #NGADA . Kwanza kila ukikutana naye anataka aongee yeye tu maneno yake ya #LAWAMA na kujiona anaonewa ili hali ana #HAKI sana bila kujali hali aliyonayo kwa sasa. Kuna waathirik...