Skip to main content

SIKUJITANGAZA KUWA MIMI BADO NI BIKIRA ILA ILITOKEA TUU-CHEMICAL






Rapper Chemical amedai kauli yake ya kuwa yeye bado ni bikira (bado hajaupoteza usichana wake) umewafanya wanaume wengi kumtokea huku watu wengine wakijitokeza na kutaka kumtafutia mwanaume.

Chemical amedai wakati anatoa kauli hiyo hakudhamiria kuweka wazi suala hilo lakini alilazimika kutoa jibu hilo baada ya kuulizwa swali.
“Kiukweli toka nimefanya vile napata comment nyingi sana wengine wanasema sikuwa na busara kufanya vile,” Chemical alikiambia kipindi cha FNL cha EATV. “Lakini nataka kuwaambia kwanza sikujitangaza ila ilitokea tu baada ya kuulizwa vitu ambavyo inawezekana siwezi kuvijibu,”
Aliongeza, “Lakini napenda kuwaonyesha watu tusilazimishe kwa kuwa wewe umepitia kitu fulani wote tunatakiwa kuwa tumepitia jambo hilo, mimi najua background yangu niliyotokea siku zote na focus kwenye ‘Career’ yangu sitaki kitu chochote kiniharibie hasa sijui mwanaume ajae kuniharibia maisha yangu” alisema Chemical
Mbali na hilo Chemical aliweka wazi juu ya watu ambao wamekuwa wakijitokeza kutaka kumtafutia mwanaume na kusema yeye hana shida hata wakimtafutia mwisho wa siku yeye lazima ampime kuona kama anamfaa au hafai
USIKOSE KUANGALIA VIDEO HII NA SUBSCRIBE ACCOUNT YA YOUTUBE HAPA CHINI


Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.