Skip to main content

MANENO YA RAPA NIKKIMBISHI KUHUSU HALI YA CHID BENZ

Leo December 30, 2016 rapa Nikki Mbishi amefunguka kuhusu watu wanaolalamika kuhusu hali ya rapa anayetawa kuwa mkali wa Freestyle Tanzania, Rashid Makwilo a.k.a Chid Beenz a.k.a Chuma a.k.a Chid wa Ilala na kusema kwamba watu wengi wanaolalamika hawajui ukweli kuhusu Chid.
Nikki Mbish amesema tatizo la Chid Benz amekuwa hataki kusikia lolote kutoka kwa watu wanaohitaji kumsaidia, na kila akisaidiwa kupelekewa Rehab anatoroka, lakini pia watu wanaompiga picha wengi wao hawajui matatizo ya Chid na wanataka kuonekana tu walikuwa naye.
Unaweza kusoma kila kitu alichokiandika hapa chini kupitia Instagram.
“Siwezi kupost hata picha yake wala video maana ni #FEDHEHA tu ila ukweli ni kwamba nafsi ya #CHID_BENZ haiko tayari kusaidiwa kuacha #NGADA.  Kwanza kila ukikutana naye anataka aongee yeye tu maneno yake ya #LAWAMA na kujiona anaonewa ili hali ana #HAKI sana bila kujali hali aliyonayo kwa sasa.
Kuna waathirika wengi wa madawa ya kulevya hawajawahi hata kujaliwa kwa kupata hata msaada wa kupelekwa #REHAB lakini Chid alishikwa mpaka na vitu Airport na yakasawazishwa.  Je,angeshikwa mtu mwingine si ndo ingekuwa n’tolee? He took it for granted, he is ungrateful… Wasaidizi wamechoka pia.  #NINI_KIFANYIKE na yeye hayuko tayari? – Nikki Mbishi


nikki-mbish

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.