Jay Z na Beyonce ni moja ya couple katika Ulimwengu wa burudani, yenye uwezo wa kupata chochote wanachokihitaji katika kufurahia maisha yao. Wawili hao wamedaiwa kununua jumba la kifahari mjini Los Angeles. Kwa mujibu wa Page Six, maamuzi ya wawili hao kununua jumba hilo la kifahari, limetokana na kubadilisha mazingira kutoka New York ambapo wanaishi sasa, kwa ajili ya kuwakaribisha watoto wao mapacha ambao wanatarajiwa kuzaliwa Juni mwaka huu. Jumba hilo linadaiwa kuwagharimu kiasi cha dola milioni 135 likiwa lina vyumba nane vya kulala, mabafu 11, madirisha yasiyopitisha risasi, chumba cha habari, sehemu ya studio, gereji yenye uwezo wa kuchukua magari 15 kwa wakati mmoja na mengine. Kama ni kweli Jay na Queen Bey watahamia kwenye jumba hilo watakuwa ni majirani wa mastaa wengine kama muigizaji, Salma Hayek, muimbaji Tom Jones na bosi wazamani wa Disney, Michael Eisner.