Baada ya ugonjwa wa mafua ya ndege kugundulika nchi jirani ya Uganda baada ya kuwepo kwa vifo vingi vya ndege pori katika maeneo ya Lutembe beach, Masaka, Kachanga, Bukibanga na Bukakata na vifo hivyo kutokea kwa baadhi ya ndege wafugwao (kuku na bata) na inahisiwa kuwa ndege hao wamepata virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa ndege pori wanaohama kutoka nchi za Ulaya. Baada ya taarifa hizo Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto leo January 18 2017 imetoa taarifa kuhusu kuwepo kwa virusi vya mafua makali ya ndege katika nchi jirani ya Uganda. Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa maeneo yalioathirika ni maeneo yanayozunguka ziwa Victoria pamoja na ziwa lenyewe. Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya imesema kuwa hadi sasa hakuna binadamu yeyote aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo huko nchini Uganda hivyo wametoa tahadhari kuwa kuna uwezekano mkubwa wa ugonjwa kusambaa kwa binadamu ikiwa hatua madhubuti za kujikinga hazitazi...