Mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo ameongoza kwa kuwa mwanasoka mwenye kipato zaidi kwa msimu wa 2016-17 hadi sasa. Ronaldo tayari ameingiza kitita cha pauni milioni 75.62 na amempiga bao mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona ambaye amepata pauni milioni 66.12. Fedha hizo zinatokana na mshahara, posho, malipo ya motisha na mikataba ya matangazo na Ronaldo anaonekana amepanda haraka baada ya kushinda Ballond’Or. Kiungo mwingine wa Barcelona, Neymar, yeye anaonekana kumpiga bao Gareth Bale wa Madrid. Listi hii hapa MCHEZAJI TIMU KIPATO Cristiano Ronaldo Real Madrid Pauni 75.62m Lionel Messi ...