Skip to main content

Posts

Showing posts from March 16, 2017

Wanasayansi wagundua kiumbe kingine kinachobadilika rangi kama Kinyonga

Unaweza kutoamini lakini inapofikia wakati ikathibitishwa ni lazima kuamini. Tumekuwa tukiamini kwa kusikia na wakati mwingine kwa kuona kwa macho yetu kuwa   Kinyonga   ndiye kiumbe Pekee anayeweza kubadilisha rangi yake kulingana na mazingira. Leo nimekutana na hii ya Wanasayansi wa   Argentina  ambao wamemgundua   Chura   wa kwanza duniani mwenye uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi yake anapopigwa na mwanga wa jua ambapo wanasayansi hao walisema   Chura   huyo hubadilika kutoka rangi ya   Kahawia   kwenda rangi ya   Kijani   iliyofifia au   Blue   pindi anapokutana na mwanga mkali wa jua. Wanasayansi hao walisema   Chura   huyo hukoza rangi zaidi anapokutana na jua kali zaidi na rangi yake huzidi kupungua akipigwa na mwanga mdogo wa jua wakidai ni jambo ambalo hawakulitegemea ukiwa ni ugunduzi mpya kwao kwa kuwa ni mara chache viumbe wa ardhini kuwa na uwezo wa kubadilisha rangi ya ngozi zao. ...

Kidboy: Kumtukana Harmorapa ni sawa na kumpiga chura teke

Pamoja na baadhi ya wadau na mashabiki wa sanaa nchini kuendelea kumtupia maneno machafu msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa, msanii huyo anaonekana kuendelea kung’ara. Producer na mtangazaji mkongwe wa redio na mmiliki wa Tetemesha Production, Sandu Mpaka aka Kidboy, amesema licha ya changamoto ambazo anakutana nazo msanii huyo za kutukanwa na baadhi ya wadau mbalimbali, hali hiyo ndiyo inayosababisha vyanzo tofauti kumzungumzia na watu kumuelewa zaidi. Akizungumza na mtangazaji Manoni MJ wa Pili wa CG FM ya Tabora, Kid amedai kuwa Watanzania wanahitaji burudani za aina tofauti hivyo watu hawatakiwi kuhoji juu ya suala la Harmorapa kupewa airtime kwenye vyanzo vya habari. Msikilize zaidi Kid hapo chini. Audio Player

Bonucci: Napenda tukutane na Barcelona, Bayern ni hatari zaidi

Mchezaji wa klabu ya Juventus Leonardo Bonucci amefunguka kuwa angependa kukutana na Barcelona kwenye mechi za robo fainali ligi ya Mabingwa msimu huu. Juventus wamefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuitoa Porto kwenye michuano hiyo, na Bonucci anatamani droo ya Ijumaa iwakutanishe na Barca ili walipize kisasi cha 2014-15 dhidi ya timu hiyo. “Klabu yetu ni miongoni mwa klabu bora za Ulaya na sasa ni muda wa kwenda mbali iwezekanavyo. Leicester imeshangaza wengi katika michuano lakini mimi binafsi ningependa kukutana ba Barcelona,” Bonucc alisema hayo katika tovuti ya klabu hiyo. “Kukutana na klabu iliyotunyima fursa ya taji miaka miwili iliyopita litakuwa jambo la maana kubwa kwetu. Baada ya kuishangaza PSG, naweza kusema katika timu zilizobaki Barca wapo katika hali nzuri na wanajiamini. “Ambaye hatutaki kukutana naye? Bayern Munich. Kila tunapokwenda [Carlo] Ancelotti anajua namna ya kushinda, kama Guardiola. Ni vema kukutana na Bayern kwenye mechi moja tu ya fainal...

T.I. na Bow Wow wamporomoshea matusi mazito Trump

T.I. na Bow Wow wamemkingia kifua Snoop Dogg kwa kuumporomoshea matusi mazito Rais wa nchi hiyo, Donald Trump. Hatua hiyo ilikuja baada ya Trump kumkosoa Snoop kwa kumkejeli kwenye video ya wimbo wake ambayo inaonesha akimpiga risasi mtu anayefanana na Rais huyo. “Can you imagine what the outcry would be if @SnoopDogg, failing career and all, had aimed and fired the gun at President Obama? Jail time,” aliandika Trump kwenye Twitter. Baada ya kauli hiyo, Bow Wow alimuambia Trump: Ayo @realDonaldTrump shut your punk ass up talking shit about my uncle @SnoopDogg before we pimp your wife and make her work for us.” Naye T.I. ameandika kwenye Instagram:   “@snoopdogg is a Fuckin Legend u Fucking Tangerine Tanned Muskrat scrotum skin, Lacefront Possum fur Wig wearing, Alternative fact, Atomic Dog diarrhea face ass man,” he wrote. “Leave our legends names out ya fuckin old ass puppy piss smelling ass mouth & continue to focus on dividing minorities,building barriers, ali...