Pamoja na baadhi ya wadau na mashabiki wa sanaa nchini kuendelea kumtupia maneno machafu msanii wa muziki wa kizazi kipya Harmorapa, msanii huyo anaonekana kuendelea kung’ara.
Producer na mtangazaji mkongwe wa redio na mmiliki wa Tetemesha Production, Sandu Mpaka aka Kidboy, amesema licha ya changamoto ambazo anakutana nazo msanii huyo za kutukanwa na baadhi ya wadau mbalimbali, hali hiyo ndiyo inayosababisha vyanzo tofauti kumzungumzia na watu kumuelewa zaidi.
Akizungumza na mtangazaji Manoni MJ wa Pili wa CG FM ya Tabora, Kid amedai kuwa Watanzania wanahitaji burudani za aina tofauti hivyo watu hawatakiwi kuhoji juu ya suala la Harmorapa kupewa airtime kwenye vyanzo vya habari.
Msikilize zaidi Kid hapo chini.
Comments
Post a Comment