Mchezaji wa klabu ya Juventus Leonardo Bonucci amefunguka kuwa angependa kukutana na Barcelona kwenye mechi za robo fainali ligi ya Mabingwa msimu huu.
Juventus wamefanikiwa kutinga robo fainali baada ya kuitoa Porto kwenye michuano hiyo, na Bonucci anatamani droo ya Ijumaa iwakutanishe na Barca ili walipize kisasi cha 2014-15 dhidi ya timu hiyo.
“Klabu yetu ni miongoni mwa klabu bora za Ulaya na sasa ni muda wa kwenda mbali iwezekanavyo. Leicester imeshangaza wengi katika michuano lakini mimi binafsi ningependa kukutana ba Barcelona,” Bonucc alisema hayo katika tovuti ya klabu hiyo.
“Kukutana na klabu iliyotunyima fursa ya taji miaka miwili iliyopita litakuwa jambo la maana kubwa kwetu. Baada ya kuishangaza PSG, naweza kusema katika timu zilizobaki Barca wapo katika hali nzuri na wanajiamini.
“Ambaye hatutaki kukutana naye? Bayern Munich. Kila tunapokwenda [Carlo] Ancelotti anajua namna ya kushinda, kama Guardiola. Ni vema kukutana na Bayern kwenye mechi moja tu ya fainali ambapo jambo lolote linaweza kutokea.”
Juve kwa sasa wanaongoza ligi ya Serie A, wakiwa na jumla ya pointi 70 katika mechi 28 ambazo wamecheza.
Comments
Post a Comment