Skip to main content

Posts

Showing posts from December 31, 2016

POLISI WAMTIA MBARONI ALOYEMCHOMA MKULIMA MKUKI MDOMONI

Wafugaji wa kijiji cha Changalawe kata ya Masanze wilaya Kilosa mkoani Morogoro walioyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kufuatia tukio la mkulima Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni hatimaye wamerejea makazini kwao huku wakilalamikia baadhi ya mifugo yao kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Wakizungumza baada ya kurejea kutoka porini walikojificha kwa siku tano wafugaji hao wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wamesema mtuhumiwa wa kosa la kumchoma mkuki mkulima wamemkabidhi kwenye mamlaka husika na hivyo wameliomba jeshi hilo kuwaacha huru wale wasiokuwa na hatia. Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema hawatasita kuwakamata wafugaji wote wanaoendelea kusababisha uvunjifu wa amani katika wilya ya Kilosa. Nao baadhi ya wakulima wamesema kijiji hicho kimekumbwa na hofu kubwa na kwamba familia ya ndugu Mtitu aliyechomwa mkuki nayo ilitoweka na kuomba hifadhi kwa wasa...

ALIKIBA AMESHINDA TUZO NCHIN FRANCE AKIWABWAGA DAVIDO,EDDY KENZO,SARKODIE,SERGE BEYNAUD,YEMIALADE

Fresh kutoka kushinda tuzo ya video bora ya mwaka (Aje) kwenye tuzo za Soundcity MVP za Nigeria, Alikiba ameongeza nyingine wikiendi hii. Mkali huyo ameshinda tuzo ya Chaguo la Watu (Prix du Public) kwenye tuzo za Ufaransa za Wana Music Awards zilizotolewa Ijumaa hii. “Hii ilikuwa ni tuzo pekee ambayo ilikuwa wazi kwa watu kupiga kura mwaka huu na msisimko uliozalishwa na tuzo hii umevuka matarajio yetu kwa kuwa na majadiliano zaidi ya 30,000 kwenye matangazo yetu kupitia mitandao ya kijamii,”  waandaji wa tuzo hizo Wana Corp wameandika kwenye tovuti yao. “Mshindi, Alikiba wa Tanzania aliweza kujikusanyia jamii kubwa ya mashabiki, ‘mashabiki damu wa Alikiba’ kuweza kuuchukua ushindi. Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa Alikiba akiwa na sahihi katika label kubwa ya Sony, kushinda tuzo ya kimataifa ya MTV Europe Music Awards kama ‘Best African Act’ na yote kwa yote kuwa na moja ya video bora za mwaka na Aje,” wameongeza. “The main information of this “Public Prize” is t...