Skip to main content

Posts

Showing posts from April 12, 2017

Tunda aeleza jinsi sakata la dawa za kulevya lilivyobadili maisha yake

Video queen Tunda amedai kutajwa kwake kwenye orodha ya wanaohusika na dawa za kulevya kumempa changamoto ya kuaminika nyumbani kwa wazazi wake. Mrembo huyo amekiambia kipindi cha Enewz cha EATV kuwa tangu kutajwe kwenye wahusika wa matumizi ya madawa imemfanya kubadilisha mfumo wa maisha kwa kuwa nyumbani kwa wazazi wake wamekuwa wagumu kumuelewa. “Nimebadilisha mfumo wa maisha, naishi maisha ya low profile kwa sasa ili mambo kwanza yatulie lakini nipo. Maisha ya mitandaoni nimeacha. Suala la kutajwa linaniumiza kwa sababu nyumbani haikuwa rahisi kueleweka na wazazi,” alisema Tunda. Aliongeza, “Viongozi wanadai natumia mimi ndo niseme najitetea ukweli ni vigumu mno lakini naamini kwenye ukweli uongo hujitenga pembeni ipo siku ukweli utajulikana na maisha yataendelea kama kawaida. Niweke wazi situmii madawa ya kulevya.” Tunda na baadhi ya mastaa wengine wapo nje kwa dhamana baada ya kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya.

Manara awajibu Yanga baada ya kupinga malalamiko ya Simba kwa mchezaji wa Kagera Sugar

Baada ya kamati tendaji ya Yanga kupitia kwa mjumbe wake Salum Mkemi kutanganza kupinga malalamiko ya Simba dhidi ya Kagera Sugar kwa kumtumia mchezaji wao Mohamed Fakih kwenye mechi kati ya Kagera Sugar dhidi ya Simba, afisa habari wa Simba Haji Manara ametoa taarifa rasmi akiwataka Yanga kutulia. Kuna taarifa iliyotolewa na klabu ya Yanga inayoonyesha kuishinikiza Bodi ya ligi kutokutenda haki juu ya rufani yetu dhidi ya klabu ya Kagera Sugar kwa kumchezesha mchezaji Mohammed Fakih aliyecheza dhidi yetu akiwa na kadi tatu za njano ambalo ni kosa kisheria. Taarifa hiyo ya Yanga iliomnukuu Mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Salum Mkemi aliyeoongea mbele ya waandishi huku akiwa na katibu mkuu wa klabu hiyo Charles Boniface Mkwasa iliitaka bodi kutokutoa points kwa Simba eti kwa kuwa hizo points zitawaathiri Yanga kwenye kutetea ubingwa wao ambao kwa sasa upo rehani, pia taarifa hiyo imeonyesha Yanga wanao ushahidi kuwa Fakih ana kadi mbili za njano. Klabu ya Simba inawaa...