Malkia wa Bongo Fleva nchini Lady Jaydee amefunguka kuhusu Harmorapa ambaye amekuwa akiteka vichwa vya habari kutokana na stori zake zikiwemo nyingi za kuvunja mbavu. Jaydee amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa haoni tatizo kwa rapper huyo chipukizi kwa kuwa kila msanii ana njia zake ambazo anatumia za kufikisha sanaa yake inapotakiwa kufika. “Tumuache afanye yake, unajua kila mtu ni ambavyo anaweza kuiwakilisha sanaa yake, kwahiyo mimi naona yuko poa,” amesema muimbaji huyo. Jide ameongeza kuwa alifurahi sana baada ya kuona clip ya video ikimuonyesha Harmo akitoka nduki baada ya mbunge wa Mtama, Nape Nnauye kuonyeshewa bastola Alhamisi hii SOURCE BONGO5