Tajiri huyo namba moja kwa sasa hapa nchini alitua Italia katika klabu hiyo mapema wiki hii na kufanya nao mazungumzo juu ya kuinua soka la Tanzania. Akiongea na mtandao wa Salehjembe, Dewji amesema, “Wiki hii nilifanya kikao na Juventus FC. Wanayo nia ya kuendeleza soka kwa vijana wa Tanzania. Ninatazamia kuitambulisha timu hiyo ya Italia kwa uongozi wa Simba SC ili waanze majadiliano ya jambo hilo.”
Juventus imekuwa ikishirikiana na baadhi ya nchi za Afrika katika kuendeleza mchezo huo ikiwemo Libya (wakati ikiwa tulivu), Tunisia, Morocco na Misri.
ANGALIA VIDEO YA RAIS WA MISRI YALIYEFUNGWA KIFUNGO CHA MAISHA NA KUACHIWA HURU
Comments
Post a Comment