Hakuna anayebisha kwamba kwa sasa producer wa ‘Touchez Sound’ Mr Ttouch kuwa ndiye producer anayefanya ngoma nyingi za hivi karibuni ambazo zinafanya vizuri.
Mtayarishaji huyo ambaye mpaka sasa ana ngoma kama Komela ya Dayna Nyange, Mazoea ya Billnass, Kibabe ya Professor J, Nisaidie Kushare ya Jay Moe na ngingine nyingi ambazo zinafanya vizuri, ameiambia Bongo5 siri ya kutengeneza beat kali.
“Nashukuru Mungu kama mashabiki wameshaanza kusema ninafanya vizuri, hicho ni kitu kizuri sana ambacho kila producer anakitaka,” alisema Mr Ttouch. “Kusema kweli siri ya mafanikio yangu ni kufanya kazi kwa bidii, pia watu wajue mimi siyo msikilizaji wa muziki huu wa kisasa, mimi nyimbo zangu zote nazikiliza nyimbo za zamani, ni nyimbo ambazo zinanipa mambo mengi sana,”
Aliongeza,”Mimi nasikiliza ngoma alizo-producer Master J kipindi cha nyuma, P-Funk Majani na maproducer wengine wengi wa zamani. Nikizikiliza kuna vitu fulani ambavyo navipana na vinaweza kunisaidia kuboresha kazi zangu ndio maana kila beat nikifanya watu wanasema ni kali,”
WEKA COMMENT YAKO HAPO CHINI
Comments
Post a Comment