Tarehe 24 Novemba 2016 Wizara ilizindua Cheti kipya cha Chanjo za Kimataifa kijulikanacho kama Cheti cha Chanjo ya Homa ya Manjano ili kuendana na maboresho ya kipengele cha 7 cha Kanuni za Afya za Kimataifa za mwaka 2005. Lakini pia, zoezi hili lililenga kukabiliana na kusambaa kwa vyeti vya kugushi (feki) ambavyo watu wamekuwa wakivipata bila kupata chanjo, hali ambayo ilitishia Afya ya Jamii dhidi ya ugonjwa huo. Kwasababu hizo, Wizara iliona ni vema kufanya mabadiliko ya cheti hicho, ambapo wenye vyeti vya zamani wanabadilishiwa na wale wanaopata chanjo wanapewa cheti kipya. Wizara inapenda kutoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo kama ifuatavyo. Kabla ya kuanza matumizi ya vyeti vipya, wastani wa wasafiri 800 walikuwa wanapatiwa chanjo kwa mwezi kupitia vituo vilivyoruhusiwa na Wizara. Baada ya kuzindua vyeti vipya na kuongeza udhibiti wa vyeti feki idadi ya wanaopata chanjo imeongeza kutoka 800 hadi 2,445 kwa mwezi ikiwa ni ongezeko la mara 3 ya waliokuwa wanachanja hapo ...