Bi Abd El Aty kutokea Misri alifanyiwa upasuaji katika hospitali ya Saifee miezi miwili iliyopita, ili kupungua kutoka uzito wa kilo 500 hadi 250 kwa sasa.
Hospitali hiyo imesema mama huyo, sasa anaweza kuketi kwenye kiti cha magurudumu na kukaa chini kwa muda kinyume na hali ya awali.
Abd El Aty alifanyiwa upasuaji unaojulikana kama ‘bariatric’ na kundi la madaktari wa India wakiongozwa na Daktari Muffazal Lakdawala.
Upasuaji wa ‘Bariatric’, hufanyika wakati mtu anapokua na unene kupita kiasi na ikiwa hali hiyo inatishia maisha yake.
Hospitali hiyo inasubiri mwanamke huyo kupunguza uzani zaidi ili kuchunguzwa zaidi kuhusu hali ya kiharusi chake alichokipata tangia mdogo.
ANGALIA HISTORIA YA LUCKY DUBE HAPA
Comments
Post a Comment