Miaka 7 iliyopita, Nikikupata ya Ben Pol iliingia kwenye mawimbi ya redio na video yake iliyoongozwa na Adam Juma kubariki macho yetu. Video ya wimbo huo iliwekwa Youtube Oct 7, 2010. Wimbo huo ndio uliomzaa Ben Pol ambaye leo ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania wanaoheshimika. Miaka 7 iliyopita pia, wimbo wa pili (rasmi na wenye mafanikio) wa Diamond, Mbagala, ulitoka. Video yake, iliongozwa pia na Adam Juma na kumpa Diamond nomination ya kwanza kwenye tuzo za MTV MAMA, ya Best New Artist. Kwa Nigeria, miaka 7 iliyopita, alizaliwa pia msanii mwingine ambaye kwa sasa ni maarufu dunia nzima, Wizkid. Akiwa chini ya label ya EME inayomilikiwa na Banky W, aliachia hit single yake Holla at Your Boy (video iliweka Youtube Oct 8,2010, siku moja baada ya Nikukupata ya Ben Pol kuwekwa Youtube). Holla at Your Boy ndio unaofahamika kumtoa na kumtambulisha Wizkid katika jukwaa la muziki Afrika. Mwaka mmoja na nusu baadaye, Afrika ikapata staa mwingine, Davido ambaye wimbo Dami Duro ulio...