Miaka 7 iliyopita, Nikikupata ya Ben Pol iliingia kwenye mawimbi ya redio na video yake iliyoongozwa na Adam Juma kubariki macho yetu. Video ya wimbo huo iliwekwa Youtube Oct 7, 2010.
Wimbo huo ndio uliomzaa Ben Pol ambaye leo ni miongoni mwa mastaa wa Tanzania wanaoheshimika. Miaka 7 iliyopita pia, wimbo wa pili (rasmi na wenye mafanikio) wa Diamond, Mbagala, ulitoka. Video yake, iliongozwa pia na Adam Juma na kumpa Diamond nomination ya kwanza kwenye tuzo za MTV MAMA, ya Best New Artist.
Kwa Nigeria, miaka 7 iliyopita, alizaliwa pia msanii mwingine ambaye kwa sasa ni maarufu dunia nzima, Wizkid. Akiwa chini ya label ya EME inayomilikiwa na Banky W, aliachia hit single yake Holla at Your Boy (video iliweka Youtube Oct 8,2010, siku moja baada ya Nikukupata ya Ben Pol kuwekwa Youtube).
Holla at Your Boy ndio unaofahamika kumtoa na kumtambulisha Wizkid katika jukwaa la muziki Afrika. Mwaka mmoja na nusu baadaye, Afrika ikapata staa mwingine, Davido ambaye wimbo Dami Duro uliotoka October 30, 2011 ndio uliomtambulisha zaidi.
Leo hii Diamond, Wizkid na Davido wanafahamika kama wasanii wakubwa Afrika wakiwa na kundi kubwa la mashabiki nyuma yao. Lakini MTV Base kwa kutokuwa na research ya kutosha, inakuja kumweka Ben Pol (msanii ambaye kiumri katika muziki ni sawa na wasanii hao watatu) kwenye orodha ya wasanii wa kuwaangalia mwaka 2017.
Inamweka kwenye orodha moja na Rayvanny, ambaye umri wake kimuziki (katika masikio na macho ya wengi) sasa ni mwaka mmoja tu. MTV Base inamuangalia Ben Pol kama msanii aliyeanza muziki miaka miwili iliyopita. Najua, yeyote aliyependekeza jina la Ben Pol kwenye list hii ameanza kumfahamu kupitia video ya Moyo Mashine na Phone aliyomshirikisha Mr Eezi.
MTV Base haijui kuwa Ben Pol amekuwepo kitambo na amejikusanyia heshima kubwa kwenye muziki wa Tanzania na ni mmoja wa wasanii wa R&B wanaoheshimika sana.
Dhumuni la hizi list za wasanii wa kuwaangalia (artists to watch) ni kuwapa spotlight wasanii wapya wanaofanya vizuri. Ben Pol si msanii mpya. Amekuwepo kwa muda na tayari amefanikiwa kuinspire vijana wengi kimuziki. Kwa hits zingine kama Samboira, Number One Fan, Maneno, Jikubali, Unanichora, Sophia, Pete na Ningefanyeje pamoja na zingine alizoshirikishwa, Ben Pol si msanii wa kumwangalia mwaka 2017 because he has been there doing great things for a long time.
MTV Base imemkosea heshima Ben Pol kumweka kwenye orodha hii. Kama ningekuwa Ben Pol, hii nisingeichukulia kama heshima, bali ukosefu wa adabu uliotokana na watu kutofanya utafiti wa kutosha. Ili kuandaa list za kueleweka, MTV Base inapaswa kutumia watu muhimu kwenye kiwanda cha muziki katika nchi husika ili kupata watu wanaostahili. Njia za mkato kutengeneza orodha kama hii zitaishusha heshima yao. Badala yake wataendelea kuwawaweka wakongwe kwenye orodha za
Comments
Post a Comment