Skip to main content

Posts

Showing posts from April 1, 2017

Tizama macth live kati ya liverpool na everton

Moja kati ya majiji yenye historia ya mchezo wa soka nchini England ni pamoja na Merseyside, jiji ambalo linatoa team kama Liverpool   na hata  Everton . Huwa kinanuka mbaya  timu hizo zinapokutana kutokana na upinzani uliopo baina yao na mambo mengine kibao. Leo April 1  Everton   ni mgeni wa  Liverpool .  inakupa nafasi ya kuitazama LIVE game hiyo kwa kubonyeza maandishi mekundu hapa chini. Liverpool vs Everton (LIVE)

Mashabiki wa Napoli wametengeneza toilet paper zenye picha ya Higuan, kisaa …….

Kwa kawaida vilabu vingi vya soka huwa havipendi kuuziana wachezaji mahiri wakiwa wanacheza Ligi moja na mashabiki huwa hawapendi kumuona mchezaji wao anahamia upande wa mpinzani wao katika Ligi, wachezaji wanaofanya hivyo mara nyingi hupoteza heshima yao ndani ya club waliyotoka. Hii ndio imemtokea   Gonzalo Higuan   staa wa zamani wa   Real Madrid   ambaye alihama   Napoli   na kujiunga na   Juventus   timu ambayo ni mshindani wa   Napoli   katika   Serie A , mashabiki wa   Napoli   wanamuona kama msaliti na kesho April 2 2017 anarudi katika uwanja wa   Sao Paulo   wa   Napoli   kwa mara ya kwanza toka ahame timu hiyo. Hapa akiwa Juventus Kama ambavyo mashabiki huwa na heshima kwa wachezaji wao wanaondoka na kujiunga na vilabu vingine, ila kitendo cha kujiunga na   Juventus   Higuan   anahesabika kama msaliti na wameandaa toilet paper zenye picha ya mchezaji...

Linah azungumzia kuhusu idadi ya mimba alizowahi kutoa

March 31 2017 kupitia kipindi cha   The weekend chat show   Msanii wa Bongo fleva   Linah Sanga   amekiri alishawahi kutoa mimba takribani mbili kabla ya hii aliyonayo sasa hivi na anategemea kujifungua hivi karibu. Linah   amesema anajutia hilo na sababu iliyompelekea kutoa mimba hizo ni kwa sababu alikuwa anamuhofia baba yake kwakuwa hakuwa ameolewa na kudai baba yake alisha watahadharisha juu ya kubeba mimba wakiwa nje ya ndoa wajitenge wenyewe kwenye familia yao. Mtangazaji   Soudy Brown   alimuuliza   Linah   kama alishawai kutoa Mimba na majibu yake yalikuwa haya. .>>> “Yah nisiwe muongo nilishawahi kutoa mimba kipindi cha nyuma, nilikuwa naogopa kwasababu Baba yangu alikataa mtu kubeba mimba nje ya ndoa” “Mimba nimezitoa, siyo mara nyingi ila naweza kusema kama mara mbilii” : -Linah

BAD NEWS: Mashabiki wa Man United taarifa hii ikufikie kuhusu Juan Mata

Kiungo wa kimataifa wa   Hispania   anayeichezea   Man United   ya   England   Juan Mata   jina lake limerudi kwenye headlines baada ya kufanyiwa upasuaji wa groin,   Mata   ambaye mwanzoni mwa wiki hii alikuwa akilalamika mazoezini kuwa anasumbuliwa na groin amefanyiwa upasuaji. Taarifa zilizotoka usiku wa March 31 2017 kuhusu kiungo huyo ni kuwa upasuaji wake umeenda salama lakini kutokana na tatizo lake, kuna uwezekano mkubwa wa kukosa mechi zote za kumalizika za   Man United   tofauti na awali alivyotazamiwa kuwa anaweza kukosa mechi tatu tu. Juan Mata   ambaye alijiunga na   Man United   akitokea   Chelsea   mwaka 2014 , hajawahi kukosa mechi za   Man United   katika kipindi cha miaka yote mitatu aliyokuwepo klabuni hapo pasipokuwa na majeruhi, mara zote amekuwa akikosekana kwa sababu za msingi ikiwemo majeruhi. SIKILIZA NYIMBO MPYA YA RICH MORE NAN MKALI