Kwa kawaida vilabu vingi vya soka huwa havipendi kuuziana wachezaji mahiri wakiwa wanacheza Ligi moja na mashabiki huwa hawapendi kumuona mchezaji wao anahamia upande wa mpinzani wao katika Ligi, wachezaji wanaofanya hivyo mara nyingi hupoteza heshima yao ndani ya club waliyotoka.
Hii ndio imemtokea Gonzalo Higuan staa wa zamani wa Real Madrid ambaye alihama Napoli na kujiunga na Juventus timu ambayo ni mshindani wa Napoli katika Serie A, mashabiki wa Napoli wanamuona kama msaliti na kesho April 2 2017 anarudi katika uwanja wa Sao Paulo wa Napoli kwa mara ya kwanza toka ahame timu hiyo.
Kama ambavyo mashabiki huwa na heshima kwa wachezaji wao wanaondoka na kujiunga na vilabu vingine, ila kitendo cha kujiunga na Juventus Higuan anahesabika kama msaliti na wameandaa toilet paper zenye picha ya mchezaji huyo na kuziuza kama ishara ya kuwa hana thamani kwao.
Kitendo cha Higuan kuondoka Napoli na kujiunga na Juventus kwa pound milioni 75 wakati wa dirisha kubwa la usajili la majira ya joto, kulifanya mashabiki wa Napoli kuamua kuchoma jezi zake wakioneshwa hawataki kuwa na kumbukumbu yoyote ya mchezaji aliyehamia kwa wapinzania wao.
Comments
Post a Comment