Skip to main content

Posts

Showing posts from April 10, 2017

Bashe awasha moto bungeni sakata la utekwaji watu

Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema hawezi kulifumbia mambo jambo la watu kutekwa na watu wasiojulikana. Bashe ameyaanisha hayo Jumatatu hii na kusema kuwa na yeye ni mmoja wa watu wa waliotumiwa ujumbe wa vitisho ambao ulisema atafanyiwa vitendo vibaya popote alipo. Aidha Mhe Bashe ameeleza kuwa kuna kikundi kilicho chini ya idara ya usalama wa taifa kinachoendesha matukio hayo na kinaharibu heshima ya serikali na chama na ameomba ikiwezekana Bunge liunde ‘Committee’ ya kuchunguza jambo hilo. Sambamba na kuzungumza bungeni hakuishia hapo katika mtandao wa tweeter ameandika: “Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.”

Mimi Mars adai Lulu na Wema waliwahi kukataa kumpa shavu kwenye movie

Marianne Mdee aka Mimi Mars amepitia vikwazo vingi katika kutafuta tobo kama ambavyo wasanii wengine wamepitia licha ya yeye kuwa mdogo wake na Vanessa Mdee. Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Mimi alisema Lulu na Wema Sepetu waliwahi kumtosa kumpa shavu kwenye movie. “Nilishawahi kumuomba Lulu, Elizabeth Michael nakumbuka tuliwahi kuongea naye hata akina Wema kuomba kuingiza kwenye bongo movie lakini, Vanessa ndio alikuwa ananisaidia kuongea nao lakini kama walinipiga chini fulani hivi but it’s okay,” alisema. Hata hivyo Mimi hana kinyongo nao kwakuwa kipindi hicho alikuwa hajulikani na anaona ni kitu cha kawaida. Anasema wawili hao kwa sasa ni marafiki zake.

Tumeshtushwa na tukio la Roma, lazima tujue kiini chake – Dkt Mwakyembe

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amesema tukio la kutekwa kwa Roma na wenzake watatu limewashtua. Ameda kuwa hilo si jambo lililozoeleka Tanzania na kwamba ni lazima wafuatilie kujua kiini chake. Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii, Dkt Mwakyembe amesema tukio hilo linaweza kuwa limefanywa na watu wachache kwaajili ya kuvuruga mambo. “Mimi nawathamini sana vijana wangu hawa,” amesema Dkt Mwakyembe. “Hawa ni stars, hawa ndio wanainbrand Tanzania. Huyu ni bendera ya Tanzania, siwezi kukubali tukachezeachezea watu hawa kwasababu zozote zile, ndio maana nasema tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunaviruhusu vyombo vya upepelezi ambavyo vitafuatilia kwa ukaribu sana tupate majibu ya kile kilichotokea,” ameongeza. Dkt Mwakyembe amesisitiza kuwa wizara yake ipo kwaajili ya wasanii na itawalinda kwa namna yoyote na kwamba pale watakapoona hatari yoyote wasisite kumjulisha. Amesema anachosubiri ni majibu ya upepelezi ulioanza ...