Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amesema tukio la kutekwa kwa Roma na wenzake watatu limewashtua.
Ameda kuwa hilo si jambo lililozoeleka Tanzania na kwamba ni lazima wafuatilie kujua kiini chake. Akiongea na waandishi wa habari Jumatatu hii, Dkt Mwakyembe amesema tukio hilo linaweza kuwa limefanywa na watu wachache kwaajili ya kuvuruga mambo.
“Mimi nawathamini sana vijana wangu hawa,” amesema Dkt Mwakyembe.
“Hawa ni stars, hawa ndio wanainbrand Tanzania. Huyu ni bendera ya Tanzania, siwezi kukubali tukachezeachezea watu hawa kwasababu zozote zile, ndio maana nasema tushirikiane kwa pamoja kuhakikisha kwamba tunaviruhusu vyombo vya upepelezi ambavyo vitafuatilia kwa ukaribu sana tupate majibu ya kile kilichotokea,” ameongeza.
Dkt Mwakyembe amesisitiza kuwa wizara yake ipo kwaajili ya wasanii na itawalinda kwa namna yoyote na kwamba pale watakapoona hatari yoyote wasisite kumjulisha.
Amesema anachosubiri ni majibu ya upepelezi ulioanza na kwamba atahakikisha anaupata na kuusema bungeni wakati anawasilisha bajeti yake.
Comments
Post a Comment