Marianne Mdee aka Mimi Mars amepitia vikwazo vingi katika kutafuta tobo kama ambavyo wasanii wengine wamepitia licha ya yeye kuwa mdogo wake na Vanessa Mdee.
Akiongea kwenye kipindi cha Bongo Dot Home cha Times FM, Mimi alisema Lulu na Wema Sepetu waliwahi kumtosa kumpa shavu kwenye movie.
“Nilishawahi kumuomba Lulu, Elizabeth Michael nakumbuka tuliwahi kuongea naye hata akina Wema kuomba kuingiza kwenye bongo movie lakini, Vanessa ndio alikuwa ananisaidia kuongea nao lakini kama walinipiga chini fulani hivi but it’s okay,” alisema.
Hata hivyo Mimi hana kinyongo nao kwakuwa kipindi hicho alikuwa hajulikani na anaona ni kitu cha kawaida. Anasema wawili hao kwa sasa ni marafiki zake.
Comments
Post a Comment