Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe amesema hawezi kulifumbia mambo jambo la watu kutekwa na watu wasiojulikana.
Bashe ameyaanisha hayo Jumatatu hii na kusema kuwa na yeye ni mmoja wa watu wa waliotumiwa ujumbe wa vitisho ambao ulisema atafanyiwa vitendo vibaya popote alipo.
Aidha Mhe Bashe ameeleza kuwa kuna kikundi kilicho chini ya idara ya usalama wa taifa kinachoendesha matukio hayo na kinaharibu heshima ya serikali na chama na ameomba ikiwezekana Bunge liunde ‘Committee’ ya kuchunguza jambo hilo.
Sambamba na kuzungumza bungeni hakuishia hapo katika mtandao wa tweeter ameandika:
“Bunge na Serikali haiwezi kulifumbia macho jambo hili la haramu wakati Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana. Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 waliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale tulipo.”
Comments
Post a Comment