Skip to main content

ALIKIBA AMESHINDA TUZO NCHIN FRANCE AKIWABWAGA DAVIDO,EDDY KENZO,SARKODIE,SERGE BEYNAUD,YEMIALADE

Fresh kutoka kushinda tuzo ya video bora ya mwaka (Aje) kwenye tuzo za Soundcity MVP za Nigeria, Alikiba ameongeza nyingine wikiendi hii.
Mkali huyo ameshinda tuzo ya Chaguo la Watu (Prix du Public) kwenye tuzo za Ufaransa za Wana Music Awards zilizotolewa Ijumaa hii.
“Hii ilikuwa ni tuzo pekee ambayo ilikuwa wazi kwa watu kupiga kura mwaka huu na msisimko uliozalishwa na tuzo hii umevuka matarajio yetu kwa kuwa na majadiliano zaidi ya 30,000 kwenye matangazo yetu kupitia mitandao ya kijamii,” waandaji wa tuzo hizo Wana Corp wameandika kwenye tovuti yao.
“Mshindi, Alikiba wa Tanzania aliweza kujikusanyia jamii kubwa ya mashabiki, ‘mashabiki damu wa Alikiba’ kuweza kuuchukua ushindi. Mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwa Alikiba akiwa na sahihi katika label kubwa ya Sony, kushinda tuzo ya kimataifa ya MTV Europe Music Awards kama ‘Best African Act’ na yote kwa yote kuwa na moja ya video bora za mwaka na Aje,” wameongeza.
“The main information of this “Public Prize” is to see that our small website created in France can have links with a country like Tanzania thanks to Alikiba. Just for that, we say thank you to all those fans who have mobilized: a new link between Paris and Dar-Es-Salaam has been formed,” wamesisitiza.
Kwenye tuzo hiyo Alikiba alikuwa akichuana na Davido, Eddy Kenzo, Sarkodie, Serge Beynaud, Yemi Alade. Kulikuwa na jumla ya vipengele 14. Kundi la Sauti Sol nalo limeshinda kipengele cha kundi bora la mwaka.
ANGALIA HII KAMA ILIKUPITA HAPA

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.