Hit maker wa wimbo ‘Moyo Sukuma Damu’ Lameck Ditto amedai kabla hajaandika wimbo huo alianza kufanya utafiti ili kujua kazi ya moyo.
Muimbaji huyo ambaye pia ni muandishi mzuri wa nyimbo, alikiambia kipindi cha Yaliyomo Yamo Cha Radio One Stereo kuwa asingeweza kuandaa wimbo huo vizuri bila kufanya utafiti wa kile alichokizungumza.
“Kabla sijaimba Moyo Sukuma Damu, nilifanya research kujua kazi ya moyo,” alisema Ditto.
Aliongeza, “Muziki wa sasa hivi umekuwa sana, mashabiki wanasikiliza neno hadi neno, kwahiyo suala la utafiti kama unaweza kufanya ni bora ufanye ili kuboresha zaidi muziki wako,”
Muimbaji huyo ni mmoja kati ya wasanii wachache waliorudi kwa kishindo kwenye muziki baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu.
Comments
Post a Comment