Skip to main content

BURUDANIPicha: Tazama makazi mapya ya Jay Z na Beyonce


Jay Z na Beyonce ni moja ya couple katika Ulimwengu wa burudani, yenye uwezo wa kupata chochote wanachokihitaji katika kufurahia maisha yao. Wawili hao wamedaiwa kununua jumba la kifahari mjini Los Angeles.
Kwa mujibu wa Page Six, maamuzi ya wawili hao kununua jumba hilo la kifahari, limetokana na kubadilisha mazingira kutoka New York ambapo wanaishi sasa, kwa ajili ya kuwakaribisha watoto wao mapacha ambao wanatarajiwa kuzaliwa Juni mwaka huu.
Jumba hilo linadaiwa kuwagharimu kiasi cha dola milioni 135 likiwa lina vyumba nane vya kulala, mabafu 11, madirisha yasiyopitisha risasi, chumba cha habari, sehemu ya studio, gereji yenye uwezo wa kuchukua magari 15 kwa wakati mmoja na mengine.
Kama ni kweli Jay na Queen Bey watahamia kwenye jumba hilo watakuwa ni majirani wa mastaa wengine kama muigizaji, Salma Hayek, muimbaji Tom Jones na bosi wazamani wa Disney, Michael Eisner.

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.