Mtu aliyehusika kwenye shambulio la lori katika soko la Christmas, Berlin na kuuawa watu 12 siku chache zilizopita ameuawa nchini Italia.
Kijana huyo mwenye miaka 24 aliyetambulika kwa jina la Anis Amri raia wa Tunisia amedaiwa kuuawa na polisi wa mjini Milan baada ya kuwafyatulia risasi polisi waliotaka awaonyeshe vitambulisho vyake.
Imedaiwa kuwa tukio hilo lilitokea Ijumaa hii kwenye eneo la Sesto San Giovani hata hivyo mtuhumiwa huyo alifanikiwa kumuua polisi mmoja kabla na yeye kuuawa kwa kupigwa risasi.
Comments
Post a Comment