Moja kati ya jambo lililowasikitisha wengi Jumatatu hii katika mkutano ulioandaliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ni pale walipotajwa watoto wawili wa kike ambapo mmoja ana umri wa miaka 14 na mwingine 16 kuwa walikuwa wakitumia dawa za kulevya kwa takriban miaka mitano.
Wakati huo huo mtoto mmoja mwenye miaka 16 aliongeza kuwa mbali na kutumia madawa hayo lakini pia yamempelekea kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kuwa wakati mwingine ilimlazimu kujiuza ili apate fedha za kununulia dawa hizo.
Wakati huo huo Kamishna mpya wa kupambana na Madawa ya kulevya, Rogers Sianga ameahidi kuwasaidia watoto hao kwa kuwapatia huduma bora za afya ambazo zitawasaidia wasirudi tena kwenye janga hilo.
Orodha hiyo ya tatu iliyotolewa leo na Mh. Makonda ina idadi ya majina 97 ambapo kati yao amedai kuna majina ambayo yatawasha moto zaidi huku akiahidi kuwa kuna awamu nyingine nne zimebakia za kutoa majina hayo.
Comments
Post a Comment