Kampuni ya Samsung imetoa taarifa yake baada ya kufanya uchunguzi juu ya sababu ya kulipuka kwa simu zake za Galaxy Note 7.
Taarifa hiyo imebaini kuwa betri za simu hizo ndio zilizokuwa chanzo cha kulipuka kutokana na kasoro zilizojitokeza kwenye utengenezaji wa betri hizo ambazo zilitengenezwa na mbili ambapo ilitokana mwanzo katika uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa wake.
Ripoti hiyo imeongeza kuwa matatizo mengine yalitokana na betri hizo kuwa kubwa na hivyo kutokaa vizuri katika sehemu yake ya ndani ya simu. Simu hizo zilisitishwa kuuzwa mwezi Oktoba mwaka jana huku ikikadiriwa kuwa simu hizo tayari zilikuwa zimeuza kiasi cha dola bilioni 5.3 duniani kote.
Comments
Post a Comment