Ripoti mpya za Shirikisho la Kimataifa la Historia ya Soka na Takwimu (IFFHS) zimeonesha list yenye majina ya mastaa 48 bora wa soka duniani wa muda wote ambao ni wakongwe na bara la Afrika limeingiza majina ya wachezaji 7 waliofanya vizuri kwenye mchezo huo.
Wachezaji kutoka Afrika waliotajwa kwenye list hiyo ni pamoja na Nwanko Kanu (Nigeria), George Weah (Liberia), Lucas Radebe (Afrika Kusini), Mahmoud El-Khatib (Misri), Mohamed Aboutrika (Misri), Mustapha Rabah (Algeria) na Roger Milla (Cameroon).
Comments
Post a Comment