Msanii wa muziki wa hip hop Black Rhyno amedai wakati umefika wa wasanii wa muziki wa hip hop kufanya vitu ambavyo vinapendwa.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Kama Movie’ akiwa amemshirikisha Jux, amedai tayari ameshafanya muziki wa kiharakati kwa muda mrefu na muda huu ni kwa ajili ya kufanya biashara.
“Unajua muziki umekuwa ni biashara kikubwa ni kuubrand, tushafanya hizi za ‘dan Da daadah’ ila kuna wakati inabidi ufanye vitu watu wengi wanapenda,” Black Rhyno alikiambia kipindi cha Ladha 3600 cha EFM. “Ndio maana tunafanya na hizi ngoma ambazo mambo yanazungumzwa zaidi kama mahusiano.”
Black Rhyno ni miongoni kati ya marapa wakongwe ambao wanaendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa hip hop kwa muda mrefu bila kutetereka.
Comments
Post a Comment