Klabu ya Azam FC leo December 28 2016 imetangaza maamuzi ambayo hayakutarajiwa na wengi ya kuamua kuwafuta kazi makocha wake kutokea Hispania, Azam FC imewafuta wahispania waliyokuwa wanaounda benchi la ufundi la Azam FC wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandes.
Uamuzi wa Azam FC kuwafuta kazi makocha hao umefikiwa na uongozi wa klabu hiyo baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa timu hiyo, ambapo kwa siku za hivi karibuni wamekuwa hawapati matokeo ya kuridhisha.
Kocha Zeben Hernandes anaondoka Azam FC akiwa kaiongoza timu hiyo katika michezo 17, akiwa kapata ushindi michezo saba pekee, sare michezo 6 na kupoteza michezo minne, akiwa kaiacha timu hiyo nafasi ya nne katika Ligi Kuu Tanzania bara ikiwa na point 27.
Comments
Post a Comment