Ligi Kuu soka Tanzania bara imeendelea tena leo December 28 kwa Dar es Salaam Young Africans kuendelea na harakati zake za kutetea taji la Ligi Kuu soka Tanzania bara kwa kuikaribisha Ndanda FC katika uwanja wa Uhuru Dar es Salaam
.
Yanga ambao wamekuwa na rekodi sawa na Ndanda FC kwa mechi 5 zilizopita Yanga alikuwa kamfunga Ndanda mara moja na kufungwa mara moja huku wakiwa wametoka sare michezo mitatu, ila leo Yanga amefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0, magoli yakifungwa na Donald Ngoma dakika ya 4 na 21, Amissi Tambwe dakika ya 25 na Vincent Bossou.
Comments
Post a Comment