Skip to main content

DARASSA AKIFANYA YAKE MBELE YA WAFANYABIASHA WA ILALA

Hit maker wa wimbo Muziki, Shariff Thabeet aka Darassa Jumatano hii alikutana na wafanyabiashara wa soko la Ilala Boma na kuonyesha baadhi ya vitu ambavyo ataenda kuvifanya Jumamosi hii kwenye Jukwaa la Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar es Salaam.

Darassa akifanya yake mbele ya wafanyabiashara wa Ilala.

Darassa na Roma, kwa pamoja watapanda katika Jukwaa la Dar Live kwenye Mkesha wa Mwaka Mpya ili kumaliza ubishi wa nani mkali wa michano katika pambano la Nichane Nikuchane.
Akiwa kwenye Viwanja vya Karume jijini Dar, leo, Darassa aliisimamisha Ilala pale alipotoa burudani fupi ikiwa ni kionjo kabla ya shoo yenyewe kamili ya siku hiyo.
Akiongea na mashabiki wake, Darassa alisema amejipanga vizuri kuonyesha mambo mapya katika jukwaa hilo la burudani.
“Mashabiki zangu, siku hiyo ya Mkesha wa Mwaka Mpya mnachotakiwa kufanya ni kuja kwa wingi pale Dar Live kushuhudia miujiza nitakayoifanya kwani siku zote naamini huwa nafanya miujiza kila ninapopanda jukwaani.” alisema Darassa.
Naye Meneja wa Mkuu wa Kampuni ya Global Publishers ambao ni waandaaji wa pambano hilo, Abdallah Mrisho, alisema: “Shoo hii inayoenda kufanyika ni ya tofauti, kama tujuavyo Roma na Darassa kwa sasa ndiyo habari ya mjini hasa kwenye muziki wa Hip Hop, hii ni mara ya kwanza kwa Darassa kupanda kwenye Jukwaa la Dar Live, hivyo mashabiki ni fursa yenu kujumuika naye siku hiyo.”
Katika hatua nyingine, Meneja wa Dar Live na mratibu wa mpambano huo, Juma Mbizo, alisema: “Kwa kiingilio cha Sh 5,000, mashabiki watapata fursa ya kuingia na kushuhudia mpambano huo mkali ambao rasmi utaanza saa 7 mchana mpaka majogoo.”
Mbali na wakali hao kupanda jukwaani siku hiyo, pia wengine watakaotoa burudani ni pamoja na Kundi la Muziki wa Taarab la Jahazi, Juma Nature, Makhirikhiri, MC Darada, Topido, ID Classic, H-Mbizo na wengine wengi.

Comments

Popular posts from this blog

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.

MCHEZAJI WA NICE YA UFARANSA AMESEMA ALIKUA MWATHIRIKA WA UBAGUZI WA RANGI

Mchezajiwa wa klabu ya Nice ya nchini Ufaransa Mario Balotelli anasema kuwa alikuwa mwathiriwa wa ubaguzi wa rangi wakati wa mechi ya Ijumaa dhidi ya Bastia. Balotelli ambaye mchezaji hyo wa zamani wa Liverpool mwenye umri wa mika 26 aliandika katika mtandao wa kijamii akisema, ni jambo la kawaida kwamba wafuasi wa Bastia hufanya makelele ya tumbili kwa mechi yote na hakuna mtu katika idara ya adhabu anayechukua hatua? ”Kwa hivyo ubaguzi wa rangi ni sheria halali nchini Ufaransa? Ama ni Bastia pekee? Soka ni mchezo mzuri lakini watu kama wafuasi wa Bastia wanaharibu.Ni aibu kubwa”. Balotelli ambaye alicheza dakika 90 aliporudi uwanjani baada ya kutumikia adhabu yake ya mechi waliyo toka sare ya 1-1 huko Corsica. Ujumbe huo uliotumwa katika mtandao wa Instagram ulisambazwa na Nice katika mtandao wa Twitter wa klabu hiyo. Jopo la adhabu la ligi ya Ufaransa ambalo hutoa maamuzi halijatoa tamko lolote. Balotelli amesha funga mabao 10 katika mechi 15 tangu alivyo jiunga na ...

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.