Skip to main content

MUDA WA DIRISHA DOGO MOURIHNO ATAWAFUNGULIA MILANGO WACHEZAJI HAWA HAPA



Tukikaribia muda wa dirisha dogo tunategemea kuona movement ya wachezaji wengi kwenda kwenye timu mbali mbali wakiziacha timu zao za sasa hivi. Tangu afike Manchester united Mourihno amekua akisajili wachezaji ana kujaza nafasi za wachezaji wengi kwenye namba kadhaa kufanya wachezaji hao wote wakubwa wakigombania namba moja.




Pia hadi sasa bado kuna tetesi za kuleta wachezaji wapya ambao wanakuja kuongeza swala la kugombani namba. Hivi sasa Manchester united inategemewa kumkalibisha mchezaji Victor Lindelog kutkka Benfica.
Hawa ni wachezaji watano ambao huenda wasivae tena jezi ya Manchester united baada ya muda dirisha dogo kufika.
Memphis Depay.
Bila shaka huyu jamaa mwenye miaka 22 amepitia wakati mgumu kuonyesha uwezo wake ndani ya Old trafford tangu ahamie kutoka PSV. Depay amecheza dakika 22 tu tangu msimu huu wa uanze kwenye ligi. Hivi sasa anategemewa kujiunga na club ya Everton kwa mkopo ili akapate muda zaidi wa kucheza.
Marouane Fellaini
Fellaini hajawai kuwa kipenzi cha Old Trafford na umaarufu wake unatokana na mabaya ya kusababisha magoli zaidi ya kusababisha magoli ili timu yake ishinde. Aliwai kuzomewa na mashabiki lakini bado kocha Jose anaendelea kumpa namba japo kwa dakika chake. Sasa hivi ameamua kwenda zake Milan ambapo ameshaonekana maeneo hayo siku chache zilizopita.
Bastian Schweinsteiger
Huyu jamaa alitegemea maisha mazuri ndani ya Manchester united chini ya Van Gaal. Lakini baada ya kuja kocha mpya amekosa kabisa imani naye na bila shaka anatakiwa kutafuta njia nyingine. Anategemewa kwenda kwenye ligi ya marekani.
Morgan Scheiderlin
Alivyotoka Southampton vitu vingi vilitegemewa lakini haukua hivyo. Imekua ni disappointment kubwa kwa central midfielder huyu. Anategmewa kwenda pamoja na Depay kwenye club ya Everton.
Anthony Martial
Kuna asilimia chache sana kama mchezaji huyu anaweza kusepa Manchester united. Tofauti na wenzake, Martial ameonekana akifanya juhudi na kufunga magoli. Hivyo basi hakuna uhakika kama anaweza kusepa kwenye club hii au la.

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.