Mshauri mkuu wa rais Donald Trump ambaye pia ni mkwe wake Jared Kushner amefanya ziara nchini Iraq kwa mara ya kwanza wikiendi hii.
Afisa mmoja kutoka Ikulu ya Marekani ameiambia CNN kuwa Jared amesafiri na Jenerali Joseph Dunford katika ziara hiyo ambapo wanatarajiwa kurudi mapema wiki hii.
Siku chache zilizopita mshauri huyo na mkewe Ivanka Trump ambaye ameteuliwa kukalia kiti cha msaidizi wa rais asiyelipwa walitajwa kuwa na utajiri wa takribani dola milioni 740.
Comments
Post a Comment