Skip to main content

Young Killer aeleza alivyojisikia baada ya Diamond kunukuu mistari minne kwenye nyimbo zake 3 tofauti

Diamond Platnumz ni shabiki mkubwa wa Young Killer.
Na hitmaker huyo wa ‘Marry You’ si mtu anayesikiliza nyimbo za Msodoki juu juu tu, bali kwa undani kiasi cha kushika mistari kadhaa.
Mwishoni mwa wiki, Diamond alionesha wazi kuzimia mistari konde ya rapper huyo wa Mwanza kwa kuandika minne kwenye post zake nne tofauti za Instagram na Twitter.
Mistari ya Young Killer ambayo Diamond ameiandika kwenye post zake za Instagram ni pamoja na:
1. Asa Unataka kuwa mimi na mimi ntakuwa nani….?😩 (Sinaga Swagga (Part1)
2. Naskia Usingizi ni Mbolea ndiomaana tukilala tunaota…?🤔 (Sinaga Swaga Remix)
3. Ukiona Nina changamoto changa Unga tusonge Ugali… Mwisho wa siku wote tunashiba, na Mambo yanakuwa shwari (Sinaga Swagga 1)
4. Shida ingekuwa sumu basi tungekufa wengine (Kumekucha f/ Mr Blue)
“Binafsi nafarijika sababu ni [Diamond] mtu ambaye ana fan base kubwa kwahiyo anapokuwa ameshow love kwa kitu kama hicho kupost mistari yangu hata mashabiki wake pia wanakuwa wananiamini kuwa Young Killer anafanya kazi nzuri,” rapper huyo ameiambia Bongo5.
“Kwahiyo ni moja kati ya msaada, sio lazima akulipie video, akupeleke studio ukarekodi, ni kitu chochote anachoweza kukusaidia kwa namna moja ama nyingine.”
Msikilize zaidi hapo chini:
Audio Player

Comments

Popular posts from this blog

MARIO BALOTELLI BADO ANDELEZA VITUKO VYAKE

Mchezaji mtukutu Mario Balotelli bado anaendelea na vituko vyake baada ya  kupata kadi nyekundu na kutolewa nje ya dimba kwenye dakika za majeruhi wakati timu yake ya Nice ilipotoka suluhu ya 0-0 na Bordeaux. Hii ilikuwa ni katika mtanange wa Ligi Kuu ya Ufaransa maarufu kama Ligue 1. Sare hiyo ya bila kufungana inaifanya klabu hiyo ya Nice kuzidi kukaribiwa point na klabu ya soka ya Monaco kwenye msimamo wa ligi hiyo ambapo sasa inaongoza kwa tofauti ya alama 2 pekee. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Manchester City alipatiwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumfanyia rafu mbaya Lewczuk ambaye ni beki.

CARLOZ TEVEZ AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA UTOTONI

Mshambuliaji wa zamani wa vilabu vya Manchester United na City, Carlos Tevez hatimaye amefunga ndoo na mpenzi wake wa tangu utotoni, Vanesa Mansilla, mjini San Isidro, Buenos Aires nchini Argentina. Tevez amefanikiwa kupata watoto wawili na mpenzi wake huyo ambaye alianza nae urafiki tangu akiwa ana umri wa miaka 13. Carlos Tevez akiwa na mkewake na watoto wao Florencia (left) na Katie (right) naomba maoni yako kuhisiana na alicho kifanya tevez

PICHA ZA MUONEKANO WA GARI LA SIMBA SPORT CLUB

Basi la klabu ya Simba SC aina ya Yutong sasa lina muonekano mpya baada ya  wadhamini wazamani TBL kupitia Kilimanjaro kumaliza mkataba wao na timu hiyo. Mwonekano wake safari hii, kuna picha za wachezaji mbalimbali.