Lord Eyez ameonekana kukataa kiaina kusainiwa na lebo ya BANA ambayo inamilikiwa na Barakah The Prince.
Rapper huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo wake mpya ‘Hela Yangu’ aliomshirikisha Jux, amesema hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kumsaini yeye kwakuwa ni mkubwa zaidi.
“Kuna makubaliano yangu na Barakah chini ya BANA huo wino ni mimi na yeye, huo wino hamhusu mtu mwingine yeyote. Nafikiri kwa sababu hakuna mtu yeyote anaweza kuniown Lord Eyez. Hakuna mtu anaweza kumsaini Lord Eyez coz am too bigger for that,” amekiambia kipindi cha E News cha EATV.
“Nafikiri maswali yanakuwa mengi kwasababu labda watu hawakuniona Lord Eyez, hawakunipata nikizungumza. Unajua mimi sio mtu wa pele pele, mimi sio mtu wa kiki, mimi sio mtu wa media, mimi napenda muziki wangu uwe mkubwa kuliko mimi,” ameongeza.
Comments
Post a Comment