Navy Kenzo wataizindua rasmi album yao mpya, ‘Above In A Minute’ Jumamosi hii, December 31
.
Uzinduzi huo utafanyika kwenye ukumbi wa Hyatt Regency Level 8 jijini Dar es Salaam.
Nyimbo zilizomo kwenye album hiyo ni pamoja na Lini waliyomshirikisha Alikiba, Bajaj waliyomshirikisha msanii wa Nigeria, Patoranking, Done wakiwa na Mr Eazi, Morning, Bless Up wakiwa na msanii wao, Rosa Lee, Nipendelee wakiwa na kundi la Ghana, R2Bees na zingine.
Wimbo wa kwanza kutoka kwenye album hiyo ni Feel Good waliyomshirikisha Wildad ambao ulitoka na video zake. Kwa kiasi kikubwa album hiyo imetayarishwa na Nahreel huku Chizan Brain akifanya mixing na mastering.
Watayarishaji wengine waliohusika kuisuka AIM ni pamoja na Chostix aliyetayarisha wimbo ‘Done’ pamoja na DJ Moshe Buskila aliyetayarisha nyimbo mbili.
Comments
Post a Comment